Wito watolewa kwa hatua ichukuliwe kutoa msaada wa kodi nchini

Mwanaume apita mbele ya ombi katika duka, linalo omba kodi isitishwe katika kitongoji cha Newtown mjini Sydney

Mwanaume apita mbele ya ombi katika duka, linalo omba kodi isitishwe katika kitongoji cha Newtown mjini Sydney Source: AAP

Baraza lamawaziri la taifa liko chini ya shinikizo, kukamilisha miongozo ya mashauriano yakodi kati yawapangaji nawamiliki wa nyumba ambao wana athiriwa na janga la COVID-19.


Wakati amri yakuzuia watu kufukuzwa nyumbani imetangazwa, vikundi vinavyo tetea ustawi wa jamii vimesema wapangaji wanao kabiliwa kwa matatizo yakifedha, wanahitaji msaada ambao zaidi kujimudu. Makundi hayo yanataka wamiliki wa nyumba nao wasaidiwe.

Wakati huo huo waziri mkuu amedokeza kodi zautendaji za sekta, kwa wapangaji wamajengo yakibiashara wakati huu wa coronavirus.

Ila, baraza lamawaziri lakitaifa, bado halijafikia makubaliano kwa masharti husika.

Unaweza endelea kupokea taarifa mpya kuhusu coronavirus katika luhga yako kwenye tovuti hii: sbs.com.au/coronavirus.


Share