Taarifa ya Habari 31 Januari 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili.jpg

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali ya shirikisho na Victoria zime tia saini mkataba wa uwekezaji wenye thamani ya dola bilioni $2.5 kwa elimu, ambayo serikali hizo zime sema uwekezaji huo utawasaidia wanafunzi, wafanyakazi pamoja na familia.


Serikali ya shirikisho ime endelea kutetea rekodi yake ya jinsi inavyo kabiliana na visa vya ubaguzi dhidi ya wahahudi, baada ya kugunduliwa kwa vilipuzi vilivyo kuwa vime jaa ndani ya nyumba mjini Sydney pamoja na visa vya mfululizo wa uharibifu na mashambulizi ya uchomaji moto.

Jumuia ya Afrika Mashariki Jumatano imeitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuzungumza na “wadau wote”, wakiwemo wapiganaji wanaoungwa mkono na Rwanda, ili kumaliza mapigano katika eneo la mashariki mwa nchi. Wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi amewarai vijana kujiunga kwa wingi na jeshi la taifa kusaidia kupambana na waasi wa M23 wanaojaribu kukamata maeneo makubwa zaidi mashariki mwa nchi hiyo.

Ugonjwa huo umethibitishwa katika mji mkuu, Kampala, wizara ya afya ya Uganda imesema. Mwathiriwa ni muuguzi mwenye umri wa miaka 32 ambaye amekuwa anafanya kazi katika hospitali ya taifa.Wizara ya afya ya Uganda imetangaza Alhamisi kuwa Kampala inakabiliwa na mlipuko wa Ebola ambao umesababisha kifo cha mtu mmoja katika mji mkuu, Kampala.

Share