Katika siku yakitaifa ya Sorry Day na maadhimisho ya sita ya Kauli ya Uluru kutoka Moyoni, viongozi wa jamii za kwanza walijumuika katika Wilaya ya Kaskazini, ambako wali waomba wa Australia waunge mkono kura ya maoni ya Sauti yawa Australia wa kwanza Bungeni.
Siku ya kitaifa ya Sorry Day hukumbuka unyanyasaji ambao wa Aboriginal nawatu wa visiwa vya Torres Strait waliyo pitia, na ilifanywa kwa mara ya kwanza kwenye maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa ripoti ya Walete Nyumbani 1998.
Ripoti hiyo ya 1997 ilijiri kupitia uchunguzi wa serikali kwa sera za zamani ambazo, zilisababisha watoto kuondolewa kwa nguvu kutoka familia na jamii zao, kundi la watoto hao lili batizwa jina la vizazi vilivyo ibwa.