Ahadi hiyo imejiri wakati kampeni ya Ndio ime fanikiwa kuungwa mkono na gwiji wa muziki nchini Australia John Farnham, aliye toa idhini ya kampeni hiyo kutumia wimbo wake kwa jina la You’re the Voice kama wimbo rasmi wa kampeni ya Ndio.
Huo ni wimbo wa taifa wa Australia usio rasmi. Sasa, wimbo huo utatumiwa katika matangazo ya kampeni ya Ndio, ukiunga mkono uwepo wa sauti yawa Australia wa kwanza bungeni.
Matangazo hayo yana unganisha wimbo wa John Farnham 'You're the Voice' na nyakati zamabadiliko katika historia ya Australia. Matangazo hayo yata peperushwa kwenye runinga na mitandao yakijamii, kabla ya kura ya maoni itakayo fanywa Oktoba 14
Unaweza pata taarifa kamili kuhusu kura hii ya maoni, kwa kutembelea tovuti ya the voice ya SBS kupitia anwani hii:
www.sbs.com.au/voicereferendum.