Warundi waingia debeni chini ya hofu ya Coronavirus

Afisa wa tume ya uchaguzi achunguza vitambulisho vya wapiga kura, Ngozi, Burundi

Afisa wa tume ya uchaguzi achunguza vitambulisho vya wapiga kura, Ngozi, Burundi Source: AP

Raia wa Burundi wameamkia katika vituo vyakupiga kura, kutekeleza wajibu wao wakidemokrasia.


Hata hivyo, uchaguzi huo umekumbwa na ukosoaji mkubwa wengi wakihoji maarifa yakufanya uchaguzi mkuu katikati ya janga la Coronavirus. Wakosoaji hao wameweka wazi wasiwasi wao kuhusu uwezekano wa usambaaji zaidi wa virusi hivyo miongoni mwa wapiga kura.

Licha ya ukosoaji huo wagombea wote wasaba walishiriki kwa kina, katika kampeni za uchaguzi huo mkuu, kila mmoja wao akiuza sera zake kwa raia wa taifa hilo la Afrika ya Kati.

Idhaa ya Kiswahili ya SBS ilizungumza na baadhi ya warundi wanao ishi nchini Australia, kuelewa zaidi kuhusu sera na kampeni za wagombea husika. Bofya hapo juu kwa makala kamili.

 


Share