Wanaharakati waweka wazi hisia zao katika maandamano mjini Melbourne

Wanaharakati wainua mabango ya Black Lives Matter mjini Melbourne

Wanaharakati washiriki katika maandamano ya Black Lives Matter mjini Melbourne, wakipinga ubaguzi wa rangi marekani na vifo vya waaustralia wakwanza gerezani. Source: The Creative Photographer

Viongozi wa afya walitoa onyo kadhaa dhidi ya watu kushiriki katika maandamano, wakati huu wa vizuizi vya Coronavirus.


Hata hivyo, maelfu yawatu walijumuika katika maandamano hayo mjini Melbourne kuonesha mshikamano na waandamanaji wanao pinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani baada ya polisi mzungu kumuuwa mmarekani mweusi.

Waandamanaji hao walikuwa wakipinga pia mauaji ya mahabusu weusi, katika vizuizi nchini Australia.

SBS Swahili ilizungumza na mwanaharakati aliye weka wazi yaliyo jiri katika maandamano hayo mjini Melbourne, Victoria.


Share