Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews naye amesema kuvaa barakoa kunaweza sababisha tofauti kubwa kwa viwango vya maambukizi.
Jimbo la Queensland lilifungua mipaka yake kwa kila mtu isipokuwa watu kutoka Victoria wakati, jimbo la Tasmania liliamua kuchelewesha kufungua mipaka yake hadi tarehe 31 Julai. Kiongozi wa jimbo hilo Peter Gutwein amesema, anawasiwasi kuhusu virusi hivyo kusambaa kisiwani humo kutoka bara.
Nalo jimbo la magharibi Australia limeamua kuchelewesha hatua zakuregeza vizuizi vya coronavirus hadi tarehe mosi Agosti.
Uamuzi huo umejiri baada ya zaidi ya idadi yawatu wa Victoria elfu moja, kuingia katika jimbo la W.A katika wiki iliyopita.
Na unaweza pata taarifa mpya kuhusu coronavirus katika lugha yako kwenye tovui hii: sbs.com.au/coronavirus