Wakazi wa Victoria kupokea huduma ya afya ya akili bila malipo

Zahanati kuminatano za afya ya akili zimefunguliwa kwa umma ya Victoria

Zahanati kuminatano za afya ya akili zimefunguliwa kwa umma ya Victoria Source: Käännöstoimisto Transly on Unsplash

Zahanati 15 zinazo toa huduma maalum ya afya ya akili, zimefunguliwa kwa umma jimboni Victoria kuanzia Jumatatu 14 Septemba, kama sehemu ya mfuko waku wasaidia wakazi wa Victoria wakati huu wa janga.


Kutakuwa zahanati tisa kwa jina la HeadtoHelp, ambazo zita toa huduma katika vitongoji vya jiji la Melbourne, na zahanati sita ambazo zita sambazwa katika maeneo ya kanda ya Victoria.

Iwapo unahitaji au unamjua mtu ambaye anahitaji huduma ya zahaniti hizo, unaweza pokea huduma hiyo katika maeneo yafuatayo: Berwick, Frankston, Officer, Hawthorn, Yarra Junction, West Heidelberg, Broadmeadows, Wyndham Vale, Brunswick East, Warragul, Sale, Bendigo, Wodonga, Sebastopol na Norlane.

Mtu yeyote ambaye ana mashaka kuhusu afya yake ya akili, anaweza tembelea zahanati hizo binafsi au, unaweza piga imu kwa namba hii: 1800 595 212 utazungumza na mtalaam wa afya au kuunganishwa na huduma iliyo karibu yako. Unaweza pata taarifa ya ziada kuhusu huduma ya afya ya akili inayo tolewa kwenye tovuti hii: headtohelp.org.au.


Share