Kupunguza hatari, serikali ya Victoria inazindua kampeni ya chanjo kwa watu wanao fanyakazi na wazee, pamoja na watu ambao wana ulemavu.
Wataalam wa afya wamesema data halisi za dunia, zitahitajika kuamua ufanisi wa dozi moja ya chanjo yakitaifa dhidi ya aina ya coronavirus iliyo tambuliwa kutoka India.Utafiti wa afya ya umma kutoka Uingereza, ulipata mwezi uliopita kuwa dozi mbili za chanjo ya AstraZeneca na Pfizer zilikuwa na ufanisi wa 88%, dhidi ya aina mpya ya virusi hivyo. Ila takwimu hizo zili poromoka hadi 33%, wiki tatu baada ya mtu kupokea dozi moja.
Kwa hatua za misaada yaki afya ambazo zipo kwa sasa katika jibu la janga la COVID-19, katika lugha yako tembelea tovuti hii: sbs.com.au/coronavirus