Wilaya ya ACT tu, ndiyo iliyo piga kura ya Ndio kwa wingi kwa Sauti.
Ni ushindi wa kishindo wa kampeni ya La, kutoka kwa wapiga kura wengi wa Australia walio pinga uwepo wa sauti yawa Australia wa kwanza bungeni.
Ilikuwa kura ya maoni ya kwanza kufanywa nchini Australia katika muda wa miaka 24. Ifuatayo ni sauti ya mwanamke mmoja jimboni Tasmania anaye toa sababu zake zakupiga kura ya La.
Endelea kupata taarifa kuhusu matokeo ya kura ya maoni ya Sauti yawa Australia wa kwanza bungeni kutoka mtandao wa SBS, pamoja na maoni kutoka wa Australia wa kwanza kupitia runinga ya NITV.
Tembelea tovuti ya SBS Voice Referendum portal kupata makala , video pamoja na makala yaliyo rekodiwa katika zaidi ya nchi 60, au unaweza sikiza taarifa mpya za habari pamoja na uchambuzi, nakupata burudani bure, kwenye tovuti ya Voice Referendum hub on SBS On Demand.