App hiyo ambayo iliundwa na shirika la Western Health pamoja na CSIRO, inaruhusu uchunguzi kwa wagonjwa kufanywa pamoja na wanachama wa jamii katika lugha 10.
Martin Foley ndiye waziri wa afya wa Victoria, amepongeza mashirika hayo ya Western Health na CSIRO, kwakupata njia mpya zakusaidia wagonjwa wenye tamaduni na lugha tofauti. Shirika la Western Health limesema, app hiyo ya CALD Assist app ina nafasi muhimu ila, haiku undwa kwa ajili yakuchukua nafasi yawakalima.
Kwa sasa app hiyo inatumiwa katika lugha 10. Baadhi ya lugha hizo ni: Kiarabu, Cantonese, kiCroatia, kiGiriki, kiItaliano, kiMacedonia, Mandarin, kiSerbia, kihispania na kiVietnam, ila kuna matumaini ya kuongeza lugha zingine pia.
Unaweza endelea kupokea taarifa mpya kuhusu coronavirus katika lugha yako kwenye tovuti hii sbs.com.au/coronavirus