Takwimu kutoka Huduma za Australia zinaonyesha kuwa jumla ya huduma za ushauri wa madakatri za telehealth ziliongezeka kutoka milioni 1.3 mnamo Machi hadi milioni 5.8 mwezi Aprili. Unaweza kutumia vizuri zaidi huduma hiyo ya telehealth kwa maandalizi kadhaa rahisi.
Watu nchini Australia lazima wakae umbali wa mita 1.5 kutoka kwa wengine. Angalia masharti ya serikali yako kwenye vikwazo vya mikusanyiko.
Ikiwa unaamini unaweza kuwa umeambukizwa virusi, piga simu kwa daktari wako (usitembele) au wasiliana na Simu ya kitaifa ya Taarifa za Afya ya Virusi vya Corona kupitia namba 1800 020 080.
Kwa usaidizi wa bure wa kibinafsi wa karibu kwa saa 24/7 kwa simu, piga simu Lifeline kwa namba 13 11 14 au Beyond Blue kwa namba 1300 22 4636. Ikiwa unahitaji mkalimani, piga Huduma ya kitaifa ya Kutafsiri na Ukalimani namba 131 450 na uliza kuunganishwa na huduma uliyopendelea.
Ikiwa unahangaika kupumua au unahitaji huduma ya dharura ya matibabu, piga simu 000.