Sheria za usalama za Australia zina piga marufuku baadhi ya bidhaa ambazo zinaweza onekana kama hazina hatari kuingizwa nchini ila, bidhaa hiza zinaweza kuwa na madhara mabaya kwa mazingira yetu pamoja na kilimo.
Uki kamatwa unajaribu kuleta bidhaa hizo nchini bila kusema unazo, watu wanaweza pewa faini nzito na hata viza zao zinaweza futwa. Kwa taarifa ya ziada kuhusu aina ya bidhaa ambazo unaweza leta Australia, tembelea Tovuti ya Idara ya Kilimo, Maji na Mazingira.
Na kama unapanga kuleta pombe, sigara, vifaa vyaki elektroniki pamoja na vitu vingine vya thamani kama vito, tazama tovuti ya Idara ya Maswala ya Nyumbani ya Australia.