Unafanyaje mipangilio ya uzazi baada yakuachana na mchumba wako?

Family court

Source: SBS

Chini ya sheria ya Familia, haki za ustawi wa watoto huongoza mazungumzo yote ya uzazi, baada ya wanandoa kutengana au kupata talaka.


Watoto wenye chini ya umri wa miaka 18, kisheria hawawezi amua ambako wata ishi. Wazazi lazima wafikie makubaliano kuhusu mipangilio ya malezi ambayo ni salama, yavitendo na inayo walenga watoto husika.


Ni mhimu kupata ushauri wa mwanasheria kabla yakufanya maamuzi yoyote, kama unahisi unashinikizwa kukubali mpangilio fulani wa uzazi na, haswa kama unapitia uzoefu wa vurugu ya familia.

Share