Tishio la janga la Corona awamu ya tatu Tanzania

Vial, blood, medical, corona, PPE, Nepali, Factsheet, COVID-19

Source: Getty Images/LEREXIS

Kamati maalumu ya Corona Tanzania, yatoa tahadhari baada ya kuwasilisha maoni juu ya mpango wa kujilinda na janga hilo.


Kamati hiyo iliundwa na Mhe Samia Suluhu Hassan mwezi uliopita ili kushughulikia masuala ya kukabiliana na janga la Corona nchini humo.

Katika taarifa yake, kamati hiyo imeishauri serikali kuweka mikakati ya kujilinda na janga hilo kubwa duniani huku ikisema, kuna tishio la viashria vya uwepo wa awamu ya tatu hivyo wanatoa ushauri kwa serikali kuanza kuweka mikakati ya kujizatiti katika kupambana na janga hilo.

Kamati hiyo pia imeishauri serikali hiyo ya Tanzania kupitia vyombo vyake kulishughulikia suala la chanjo kwa kujiunga na mpango wa covax.

Zaidi, sikiliza kwa kugonga hapo juu.


Share