Bw. Museveni pia ametoa agizo kwa polisi kuwakamata wanasiasa watakaotoa misaada ya chakula kwa jamii na kushtakiwa kwa ''jaribio la mauaji.''
Serikali ya shirikisho imetangaza mfumo wa ruzuku ya mshahara, kwa ajili yakupunguza idadi ya ajira zinazo potezwa kwa sababu ya janga la virusi vya corona. Waziri mkuu Scott Morrison amesema serikali itatoa ruzuku ya $1500 kila wiki mbili kwa kila mfanyakazi, kwa biashara ambayo inasitisha kazi katika miezi sita ijayo.
Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia unaopambana na kundi la waasi wa Kihuthi nchini Yemen umefanya mashambulizi kadhaa leo dhidi ya mji mkuu Sanaa, ambako mashambulizi kama hayo yamekuwa adimu katika miezi ya hivi karibuni kutokana na juhudi zinazoongozwa na Umoja wa Mataifa za kupunguza hali ya kuongezeka ya kivita.