Serikali ya Rwanda nayo imetangaza kuchukua hatua kadhaa za dharura kukabiliana na janga la coronavirus, saa kadhaa baada ya kutangaza kwamba raia mmoja wa India aliyewasili nchini humo Machi 8, amethibitishwa kuwa na virusi vya corona.
Katika mahojiano na Radio Rwanda, Mawaziri Anastase Shyaka wa mambo ya ndani na Dr Ngamije Daniel wa Afya, walisema kuwa hatua hizo ni pamoja na kufungwa kwa shule zote za umma na za kibinafsi, maeneo ya kuabudu na sehemu zote za umma.
Serikali ya Morrison imeonya kuwa maamuzi yote yanazingatiwa, kusaidia kukabiliana na usaambaji wa virusi vya corona. Baadhi ya maamuzi hayo yanaweza jumuisha, kufunga shule zote katika siku za usoni na hata, kusitisha matembezi na usafiri sawia na nchini Italia, Uhispani na Ufaransa.