Takriban serikali zote za Afrika zimetangaza hatua kali za kupambana na janga hilo la afya ambalo halijawahi kushuhudiwa kote duniani, ambapo mataifa yamefunga mipaka yake, kuahirisha safari za ndege na kupitisha hatua kali za karantini.
Mfalme wa soukouss, Aurlus Mabelé , mwanamziki wa kongo brazaville amefariki baada ya kuambukizwa na virusi vya korona mjini Paris, nchini ufaransa siku ya Alhamisi Machi 19, 2020.
Na ligi kuu za soka na raga nchini Australia, zashuhudia mechi bila mashabiki uwanjani, wakati viongozi wa mchezo wa AFL, waamua kuahirisha msimo mpya hadi Mei 31.