Mwekahazina wa shirikisho Josh Frydenberg anawahamasisha wa Australia wote, wanao taka rejea kazini haraka iwezekanavyo, wapakue app yaufuatiliaji ya serikali ya coronavirus.
Shirika la Afya Duniani limesihi watu kutoweka imani zao kwa dawa za mitishamba zinazotengenezwa na wenyeji kwa misingi ya kudai kukabiliana na virusi vya corona. Taarifa hiyo inaonekana kupuuzwa na baadhi ya viongozi wa Afrika. Marais wa Tanzania, Jamuhuri ya Congo, Guinea Bissau na Equatorial Guinea wote wamemaua kutuma ndege nchini Madagascar kuchukua dawa hiyo ya mitishamba.
Vita vya maneno kati ya Marekani na China vinavyo ongezeka juu ya chanzo cha mlipuko wa virusi vipya vya corona, vimesababisha thamani ya hisa kwenye masoko ya Ulaya kuanguka wakati ikianza shughuli za biashara wiki hii.