Meli hiyo ilitia nanga katika bandari ya Sydney tarehe 19 Machi na, imekuwa kiini kikubwa cha maambukizi ya virusi vya korona pamoja na vifo nchini.
Jumuiya ya nchi zinazosafirisha mafuta kwa wingi duniani OPEC na Urusi wameahirisha mkutano uliokuwa ufanyike kesho Jumatatu kujadili kupunguza uzalishaji wa mafuta.
Rais wa Malawi na mawaziri wote nchini humo watakatwa asilimia kumi ya mishahara yao ya miezi mitatu ili kupata fedha za kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona. Na mishahara ya rais wa Kenya na naibu wake kukatwa kwa asilimia 20, kukabiliana na mlipuko wa corona nchini humo