Mawaziri wa fedha wa kundi la mataifa yenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani G20, leo wamekubaliana kuandaa mikakati ya pamoja ya kukabiliana na janga la virusi vya corona.
Watu wawili wapya wathibitishwa kuwa na virusi vya corona Tanzania. Katika wagonjwa waliopatikana ni mwanaume mtanzania mwenye umri wa miaka 40 aliyesafiri nchi za Uswisi, Denmark na Ufaransa kuanzia Machi 5 hadi 13 mwaka huu na kurejea nchini Machi 14.
Nakamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) inaangalia uwezekano wa kuahirisha michuano ya Tokyo 2020, na imejipa wiki nne kufanya maamuzi, na ligi kuu ya soka nchini Australia, ya ahirishwa sawia na ligi zingine za michezo nchini na duniani kote.