Seneta wa jimbo la Vermont la Marekani, Bernie Sanders, Jumatatu alimuidhinisha aliyekuwa makam wa rais Joe Biden kuwa mgombea wa urais kwa chama cha Democratic.
Mamlaka za Afya nchini Tanzania zimetangaza wagonjwa wapya 17 wa virusi cya corona nchini humo. Wakati huo huo takriban wagonjwa 15 waliokuwa wakiugua virusi vya corona nchini Kenya wamepona katika kipindi cha saa 24 zilizopita, Waziri wa Afya wa nchi hiyo Mutahi Kagwe ametangaza.
Wazalishaji na washirika wa nchi zinazouza mafuta wakubaliana kufikia makubaliano na kupunguza uzalishaji kote duniani kwa takriban asilimia 10.