Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amelala hospitalini katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya afya yake kuzorota kutokana na virusi vya corona.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza marufuku ya kuingia na kutoka katika kaunti za Nairobi, Kilifi, kwale na Mombasa huku idadi ya maambukizi ya virusi vya corona ikiongezeka kwa visa 16 zaidi.