Majimbo matatu nchini Marekani yameruhusu baadhi ya maduka kufunguliwa tena baada ya hatua zilizowekwa za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona, huku idadi ya vifo nchini humo ikizidi watu 51,000.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameongeza muda wa marufuku ya watu kusafiri, na kuingia au kutoka katika mji wa Nairobi na miji mingine minne kwa muda wa siku 21. Bwana Kenyatta pia ameongeza tena muda wa amri ya kutotoka nje kuanzia saa moja jioni hadi saa kumi na moja alfajiri kwa siku 21 zaidi.
Wakati minong'ono kuhusu hali ya kiafya ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ikizidi kuongezeka picha za satelaiti zimeonyesha treni inayodhaniwa kuwa ni ya kiongozi huyo ikiwa imeegeshwa kwenye makazi yake yaliyoko pwani ya mashariki mwa nchi hiyo tangu wiki iliyopita.