Serikali ya shirikisho inaendelea kukataa kuikoa ndege ya Virgin Australia, baada yakampuni hiyo kujiingiza katika utawala wa hiari, wakati huo huo chama cha upinzani chaishinikiza serikali iokoe ndege hiyo.
Vital Kamerhe, Mkurugenzi wa ofisi ya rais na mshirika wa rais Felix Tshisekedi, bado anazuiliwa katika gereza kuu la Makala jijini Kinshasa, huku baadhi ya makada wa chama cha UNC wakijaribu kukutana na utawala kuomba kiongozi wao aachiliwe huru.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto, UNICEF, limetoa wito hii likihamasisha msaada zaidi wa karibu dola milioni 92.8 ili kupambana na janga la ugonjwa wa COVID-19 katika nchi za Mashariki ya kati na Afrika kaskazini.