Ufaransa na Ujerumani zapendekeza kuanzishwa kwa mfuko wa euro bilioni 500 wa kufadhili juhudi za kuukwamua uchumi wa Umoja wa Ulaya ulioathiriwa na mgogoro wa virusi vya corona.
Serikali ya Tanzania imeondoa zuio la ndege za kawaida za abiria kuingia na kutoka nchini humo ili kuruhusu shughuli za usafiri wa anga na utalii kuendelea kama kawaida.
Thomas Thabane ametangaza kuwa atajiuzulu kama waziri mkuu wa Lesotho kufuatia miezi kadhaa ya shinikizo baada ya kutajwa kama mshukiwa katika mauaji ya aliyekuwa mkewe.