Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amewakosoa viongozi wa nchi hiyo wanaoshughulikia janga la virusi vya corona akisema janga hilo linaonesha maafisa wengi "hata hawajidai tu kuwa wanawajibika."
Mshukiwa wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda, Felicien Kabuga, ambaye anashutumiwa kuwa mmoja wa wafadhili wakuu katika mauaji ya kiasi cha watu laki nane, alikamatwa Jumamosi karibu na mji mkuu wa Ufansa, Paris, baada ya kujificha kwa miaka 26, ilisema wizara ya sheria ya Ufaransa.
Kenya imefunga kwa muda wa siku 30 mipaka yake ya kimataifa kuenda Tanzania na Somalia kuanzia saa sita usiku wa Jumamosi 16 Mei 2020.