Taarifa ya Habari

bango la taarifa za habari la SBS

bango la taarifa za habari la SBS Source: SBS

Mtu wa tano athibitishwa kuwa na kirusi cha coronavirus nchini Australia.


Idadi ya watu walio uwawa nchini China na kirusi cha coronavirus imeongezeka nakufika watu 106, wakati idadi ya watu wapatao elfu nne wamethibitishwa kuwa wanaugua kwa sababu ya kirusi hicho.

Wananchi wa Burundi wana matumani kwamba nchi hiyo inatarajia kufungua ukurasa mpya baadae mwaka huu, siku moja baada ya chama tawala nchini humo, CNDD-FDD, kumpata mgombea (Jenerali Evariste Ndayishimiye) katika uchaguzi wa urais ulio pangwa kufanyika mwezi Mei 2020.

Huku siasa kuhusu uhamasishaji juu ya mchakato wa ripoti ya Jopo la maridhiano nchini Kenya (BBI) zikichacha, kumezuka tofauti kati ya wanasiasa wakuu nchini Kenya kuhusiana na mbinu na njia za kufuata katika kufanikisha suala hili.

 

 


Share