Taarifa ya Habari 9 Novemba 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Serikali ya Queensland imetangaza ita ondoa sheria za coronavirus kwa watu ambao wame pata chanjo kamili, na biashara pamoja nakuweka vizuizi kwa matembezi hospitalini kwa watu ambao hawaja chanjwa kuanzia mwezi ujao.


Katika siasa zakitaifa upinzani wa shirikisho umeukosoa mfuko wa uwekezaji wa serikali kwa gari za umeme, kwakuto jumuisha ruzuku au motisha za kodi kufanya gari hizo zinunuliwe kwa bei nafuu. Uwekezaji wa dola milioni 250 wa mafuta ya usoni na mkakati wamagari wa serikali ya mseto, utawekeza vituo vyakuweka nishati ndani ya gari katika nyumba elfu hamsini, biashara mianne pamoja na sehemu elfu moja za umma. Uwekezaji huo utaboresha pia mfumo wa umeme wa Australia, kuuwezesha kukabiliana na takriban magari ya umeme milioni moja lakisaba yanayo tarajiwa barabarani kufikia mwaka wa 2030.

Kiongozi wa waasi anayepambana na wapiganaji wa serikali, amesema vikosi vyake vipo karibu na mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, na vinatayarisha mashambulizi mengine, akitabiri kwamba mapigano yatamalizika hivi karibuni huku wanadiplomasia wakiendelea na majadiliano ya kujaribu kusitisha mapigano. Jeshi la OLA pamoja na washirika wake wa Jeshi la ukombozi wa jimbo la Tigray TPLF katika wiki za hivi karibuni wamedai kupata ushindi kwa kudhibiti baadhi ya miji na hawajaondoa uwezekano wa kuukamata pia mji mkuu, Addis Ababa.

Mizoga ya mifugo iliyonyauka ni ukumbusho kwamba ukame umeingia tena kaskazini mwa Kenya, ikiwa ni hali ya hivi punde zaidi katika mfululizo wa majanga ya hali ya hewa yanayokumba Pembe ya Afrika. Wakati viongozi wa dunia wakihutubia mkutano wa kilele wa hali ya hewa wa kimataifa huko Glasgow, Scotland wafugaji wanatazama wanyama wao wakiteseka kwa ukosefu wa maji na chakula.


Share