Taarifa ya habari 8 Septemba 2020

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Uchunguzi kwa mradi wa karantini ya hoteli ya jimbo la Victoria, umesikia ushahidi kuwa mradi huo uliandaliwa kwa kasi na hatimae ulifeli kutekeleza mahitaji ya wasafiri waliorejea.


Madaktari waliokuwa wakimtibu kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny wanasema kwamba amepata fahamu na kwamba hali yake tangu alipopatiwa sumu imeimarika.

Maafisa usalama wa Ethiopia Jumatatu waliwazuia waandishi wa habari kusafiri kuelekea mkoa wa kaskazini wa Tigray kuripoti uchaguzi wa mkoa ambao serikali imeuita kuwa ni kinyume cha katiba.

 

 


Share