Taarifa ya habari 7 Juni 2020

Bango la taarifa za habari za dunia la SBS

Bango la taarifa za habari za dunia la SBS Source: SBS

Waziri wa fedha wa Australia akataa kubadili kauli yake, iliyo wakosoa waandamanaji wa haki zakiraia


Katika kile kinachoelezwa kuwa ni maandamano makubwa zaidi kushuhudiwa dhidi ya ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi, maelfu ya waandamanaji wameshiriki nchini Marekani na maeneo mengine ya ulimwengu.

Serikali ya Kenya imeongeza muda wa kutotoka nje usiku nchi nzima kwa siku nyingine 30, amri iliyokuwa imewekwa kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa COVID-19.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limelaani vikali shambulizi ambalo limeua watu 16, wakiwemo wasichana watano walio na umri wa chini ya miaka 15, Juni 3 katika jimbo la Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).


Share