Rais wa Marekani, Donald Trump ameruhusiwa kutoka kwenye hospitali ya kijeshi ya Walter Reed alikokuwa amelazwa kwa siku tatu akitibiwa ugonjwa wa COVID-19.
Jumuia ya Afrika Mashariki Jumapili ilimuidhinisha waziri wa Spoti na utamaduni wa Kenya, Amina Mohamed, kama mgombea wao katika uongozi wa Shirika la Biashara Duniani (WTO). Hatua hiyo inaongeza uwezekano wa kupata mwanamke wa kwanza katika historia kuliongoza shirika hilo.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi yupo mjini Goma, katika eneo ambalo limeendelea kushuhudia utovu wa usalama katika kipindi kirefu kutokana na kuwepo kwa makundi ya waasi, yanayoendelea kushtumiwa kutekeleza mauaji ya raia.