Chama cha upinzani jimboni NSW kimesema kitaunga mkono, mpango wa serikali ya jimbo hilo kuwa na kifaa cha karantini kinacho wekezwa na serikali ya madola. Hatua hiyo imejiri baada ya serikali ya Victoria kufikia makubaliano na serikali ya shirikisho, kujenga kituo chenye vitanda miatano pamoja nakuongeza nafasi katika mfumo wake wa sasa wa karantini.
Kundi la viongozi wa kikabila kutoka Namibia limesema kuwa limekubali ombi la Ujerumani la kuwalipa fidia pamoja na kukiri kuwa mauaji ya maelfu ya watu yaliyofanyika mwanzoni mwa karne ya 20 yalikuwa ya kimbari. Ujerumani imeiomba msamaha Namibia kupitia kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje Heiko Maas. Wanahistoria wanasema kuwa Jenerali Lothar von Trotha alipotumwa na Ujerumani kuzima uasi kutoka kwa kabila la Herero, aliamuru vikosi vyake kulitokomeza kabila zima. Zaidi ya watu 65,000 wa kabila la Herero waliuwawa pamoja na wengine 10,000 kutoka kabila la Nama.
Muhubiri maarufu wa Nigeria TB Joshua amefariki. Taarifa iliotolewa na kanisa lake la SCOAN siku ya Jumapili alfajiri imethibitisha kifo cha Muhubiri TB Joshua. Muhubiri huyo maarufu kutoka nchini Nigeria amefariki akiwa na umri wa miaka 57. Siku ya Jumamosi tarahe 5 Juni 2021, mtume TB Joshua alizungumza katika mkutano wa runinga ya Emmanuel. ''Kila kitu kina wakati wake - tunapokuja hapa na kuomba na tutarudi nyumbani baada ya utumwa''.