Mashabiki wa Julian Assange, mchapishaji na muasisi wa mtandao wa Wikileaks waliokua nje ya mahakama mjini London wamefurahia uamuzi wa Jaji Vanessa Baraitser wa Uingereza wa kutompeleka Marekani kukabiliwa na mashtaka ya ujasusi, kwa kuchapisha waraka za siri kwenye mtandao wake. Jaji Baraister anasema amechukua uamuzi huo kutokana na hatari ya uwezekano wa Assange kujiua.
Idadi kubwa ya watu waliopigwa risasi wakati wa maandamano yaliyotokea Uganda mnano mwezi Novemba mwaka uliopita 2020 baada ya kukamatwa kwa mgombea urais Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, walikuwa na umri kati ya miaka 14 na 30. Karibu watu wote waliouawa walipigwa risasi na maafisa wa uslama kichwani, kwa shingo, mbavuni, tumboni, kifua na mgongoni.
Wakati viongozi wa nchi za Ghuba ya Uarabu wakifanya mkutano wao wa kilele leo, Saudi Arabia imeifungulia mipaka ya anga na ardhini Qatar, katika ishara ya kupunguza uhasama wa zaidi ya miaka mitatu katika ukanda huo.