Taarifa ya Habari 4 Julai 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Naibu afisa mkuu wa afya wa Australia ame wahamasisha wafanyakazi wa huduma ya wazee, wachanjwe dhidi ya COVID-19, baada ya mlipuko wa virusi mjini Sydney.


Wakaaji watatu katika kituo cha huduma ya wazee katika kitongoji cha Baulkham Hills, wanaendelea kupokea matibabu ndani ya hosptiali ya Westmead, kama tahadhari baada yakupatwa na virusi vya COVID-19.

Kiongozi wa jimbo la Queensland Annastacia Palaszczuk amewakumbusha wakaaji jimboni humo, waendelee kuvaa barakoa baada yakurekodi kesi moja mpya, inayo ungwa na jamii yawagiriki. Kesi hiyo ina aminiwa kuwa aina ya kirusi cha Alpha na, imeungwa na mlipuko wenye uhusiano na jamii yawagiriki.

Tume ya kutetea haki za binadamu ya Ethiopia (EHRC), imetilia mkazo miito ya Umoja wa Mataifa kutaka hatua za dharura zichukuliwe kuwalinda na kuwasaidia raia katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia. Jimbo hilo limekumbwa na uharibifu wa miundo mbinu muhimu huku kitisho cha njaa kikiongezeka kufuatia machafuko ambayo yamedumu kwa miezi minane sasa.


Share