Mamlaka ya kupambana na ufisadi nchini Afrika kusini ilisema Jumatu ilisema inachunguza madai ya ufisadi katika utoaji wa zabuni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kupambana na janga la Corona nchini humo.
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, kimempitisha Makamu Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, kuwania urais na hivyo kufunguwa njia kwa mahasimu wawili wakubwa nchini humo kuchuwana kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 28. Dkt John Pombe Magufuli atawakilisha chama tawala CCM katika uchaguzi mkuu.
Wanaanga wawili wa Marekani Doug Hurley na Bob Behnken wako katika safari ya mwisho na sehemu muhimu ya majaribio ya chombo cha kampuni binafsi cha SpaceX kurejea duniani, Jumapili.