Taarifa ya habari 31 Mei 2020

Bango la taarifa za habari za dunia la SBS

Bango la taarifa za habari za dunia la SBS Source: SBS

Serikali zamajimbo na wilaya zajiandaa kuinua vizuizi zaidi vya coronavirus kuanzia kesho Juni mosi.


Mwanasheria mkuu wa taifa Christian Porter ame endelea kukataa kuomba msamaha kwa mradi wakutudai madeni kwa simu, mradi ambao ulidai madeni kimakosa kutoka kwa mamia yawa Australia waliokuwa wakipokea malipo ya ustawi.

Kiongozi wa upinzani nchini Burundi, Agathon Rwasa, amewasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika wiki jana. Katika hoja yake aliyowasilisha kwenye mahakama ya katiba katika mji mkuu, Bujumbura, Rwasa amesema ana ushahidi wa kutosha kuonyesha kwamba zoezi hilo liligubikwa na dosari za kila aina.

Nchini Tanzania, maelfu wa wanafunzi wa vyuo na wale wa sekondari wanaomaliza kidato cha sita hii leo wameanza rasmi masomo yao baada ya kuwepo katika likizo ya ghafla kwa muda wa miezi miwili iliyosababishwa na kutokea kwa janga la virusi vya corona.

 


Share