Jimbo la Victoria limerekodi kesi mpya 76 za COVID-19 ndani ya jamii leo jumanne 31 Agosti. Kesi 45 kati ya hizo zime ungwa na milipuko ya sasa wakati kesi zingine 31 ziko chini ya unguzi na timu ya afya ya umma ya jimbo hilo. Kesi 36 zilikuwa zikijitenga kwa muda wote ambao, zilikuw akaitka hali ambukizi.
Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Taliban Jumatatu ameambia vyombo vya habari kwamba, ndege ya mwisho ya wanajeshi wa Marekani imeondoka kwenye uwanja wa ndege wa kimtaifa wa Kabul saa sita za usiku kwa saa za huko na kwamba vikosi vyote vya kigeni sasa vimeondoka Afghanistan. Wakati huo huo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, Jumatatu limesema kwamba linatumai kwamba Taliban watahakikisha usalama wa watu wanaotaka kuondoka nchini humo.
Wanasayansi nchini Afrika Kusini wanafuatilia aina mpya ya kirusi cha corona ambacho polepole kinazidi kusambaa katika miezi ya hivi karibuni, kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Magonjwa ya Kuambukiza NICD. Aina hiyo, inayojulikana kama C.1.2., iliripotiwa wiki iliyopita na Kituo cha Utafiti cha KwaZulu-Natal. Hata hivyo wanasema kasi yake ya maambukizi bado ni ndogo.