Kiongozi wa Victoria Daniel Andrews kwa mara nyingine ametetea sheria za janga zinazo mpa kiongozi wa jimbo hilo pamoja na waziri wa afya, mamlaka yaku tangaza janga pamoja naku amuru utekelezwaji wa vizuizi. Serikali ya Victoria imefanya mageuzi kwa muswada wake tata wa janga, kwa ajili yakupata kura ya ziada inayo hitaji ili muswada huo upitishwe bungeni. Muswada wa Afya ya umma na ustawi, uko kwenye ajenda ya nyumba ya juu bunge litakapo fanya kikao leo kwa mara ya mwisho katika ratiba ya kikao cha mwisho cha mwaka huu.
Rwanda imesimaisha kwa muda safari zake za ndege kati ya Rwanda na nchi za Kusini mwa Afrika kufuatia maambukizo ya aina mpya ya kirusi kipya cha COVID-19 Omicron. Nchi hiyo pia imeweka masharti ya kujiweka KARANTINI kwa siku saba kwa wasafiri wote wanaowasili Kigali ambao hivi karibuni walikuwa katika nchi zilizoathiriwa na corona. Kikao hicho kiliongozwa na Rais Paul Kagame. Rwanda inaungana na Umoja wa Ulaya, Marekani, Israeli, nchi za Jumuiya ya Kiarabu, Uingereza miongoni mwa nchi nyingine ambazo zimesimamisha safari zake kwenda kusini mwa Afrika.
Serikali ya kijeshi ya Chad Jumatatu imetoa msamaha kwa karibu waasi 300 pamoja na wapinzani, ikiwa hatua kubwa kuelekea shinikizo kutoka kwa makundi ya upinzani yaliyoalikwa kuhudhuria kikao cha pamoja cha kujadili hatima ya kisiasa ya taifa hilo lenye matatizo. Wakazi wengi wa mji mkuu wa N'Djamena wanasemekana kufurahishwa na msamaha huo wakiuelezea kama hatua ya kwanza kuelekea kuliunganisha taifa.