Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamehimiza juu ya mpango wa ufufuaji uchumi ulio na nguvu na madhubuti kwa ajili ya Umoja wa Ulaya, wakitaka mpango huo ujadiliwe mwezi ujao.
Rais mpya wa Burundi Evariste Ndayishimiye ameteua baraza jipya, lenye jumla ya mawaziri 15, wanaume 10 na wanawake wa 5. Baraza lazamani lamawaziri chini ya utawala wa hayati, Rais Pierre Nkurunziza lilikuwa na mawaziri 21.
Serikali ya Tanzania imetoa mwongozo mpya wa ufunguzi wa shule, vyuo na taasisi nyengine za elimu wakati ambapo taasisi zote za elimu zimefunguliwa tena kuanzia Jumatatu Juni 29,2020.