Taarifa ya Habari 3 Julai 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Mwanaume mmoja amefariki nama dazeni ya watu kuokolewa, wakati sehemu za Sydney na kanda ya Illawarra zimefurika kwa mara ya pili mwaka huu.


Australia imerekodi zaidi ya vifo elfu 10 vya UVIKO-19, wakati zaidi ya 70% ya vifo vyote vikitokea katika miezi sita iliyopita. Watalaam wameonya kuwa ugonjwa huo unaelekea kuwa sababu ya pili kubwa ya vifo nchini Australia mwaka huu nyuma ya ugonjwa wa moyo.

Rais Uhuru Kenyatta kwa mara nyengine tena amemshtumu naibu wake wa rais William Ruto huku ikiwa imesalia siku 38 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu. Akizungumza katika hafla moja katika jumba la KICC siku ya Jumamosi , rais bila kutaja jina alimshutumu naibu wake kwa kutoa ahahdi chungu nzima licha ya kwamba alikuwa na nafasi ya kutimiza ahadi hizo. Lakini akizungumza wakati wa kampeni za muungano wa Kenya kwanza huko Chuka naibu huyo wa rais alimjibu Raia Kenyatta akimtaka kukaa kando na kumpa nafasi ili kumenyana na kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga.

Raia wa afrika kusini wamebaki katika giza kutokana na kukosekana umeme kwenye makazi ya watu na biashara kote nchini humo. Tatizo la kukatika umeme limeshuhudiwa kwa miaka kadhaa sasa lakini wiki hii shirika la umeme nchini humo Eskom linalomilikiwa na serikali iliongeza muda na baadhi ya wakaazi na wafanyabiashara wamekosa umeme kwa zaidi ya saa tisa.


Share