Waziri wa afya wa shirikisho Greg Hunt amesema idadi ya maambukizi ya COVID-19 inapungua jimboni New South Wales, na kesi zingine chanya zikiwa zinatambuliwa ambazo zinajitenga. Jimbo hilo lilirekodi kesi mpya 19 za coronavirus usiku wakuamkia ila, wiki mbili za vizuizi zina endelea kwa maeneo pana ya Sydney, Central Coast, Blue Mountains, Shellharbour na Wollongong.
Maeneo ya kusini mashariki Queensland, mji wa Townsville, Palm Island, na Magnetic Island zita ingia ndani ya vizuizi vya siku tatu kuanzia saa kumi na mbili usiku wa leo. Hali hiyo imejiri baada ya jimbo hilo kurekodi kesi mbili mpya za COVID-19, moja ikimhusu mfanyakazi wa mgodi kutoka Ipswich, anaye ungwa na mlipuko wa wilaya ya kaskazini na anazingatiwa kuwa na athari ndogo.
Serikali ya Ethiopia imetangaza kusitisha mapigano Tigray - miezi nane baada ya Waziri mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed kutuma majeshi yake kukabiliana na waasi. Kundi la waasi la TPLF limedai kuuchukua mji wa Mekelle lakini serikali haijathibitisha kuupoteza mji huo. Tangazo hilo limekuja huku watu wakiripoti kushuhudia kutoona makundi ya kijeshi katika mitaa ya mji wa Mekelle.