Zaidi ya kesi 1200 zilirekodiwa jimboni humo leo jumapili 29 Agosti, pamoja na vifo sita vya ziada. Katika kijiji cha Wilcannia , takriban asilimia 11 ya wakaaji ambao wengi wao niwakiaboriginal, kwa sasa wame ambukizwa na virusi hivyo.
Wawakilishi kutoka Queensland na New South Wales wamekutana leo kujaribu kutatua, mvutano unao husu mpaka unao changiwa namajimbo hayo mawili. Jimbo la Queensland limeweka vizuizi vigumu vya mpaka dhidi ya New South Wales kama jibu kwa mlipuko wa Covid jimboni humo na, ni kundi dogo tu lawafanyakazi mhimu ambao wanaweza vuka mpaka kwa sasa. Kiongozi wa jimbo la Queensland Annastacia Palaszczuk amesema, mpangilio wa mpakani utarahisisha maisha kwa jamii zinazo athiriwa kwa hali hiyo.
Shambulio lingine dhidi ya uwanja wa ndege wa Kabul, huenda likatokea, Rais Joe Biden ameonya akisema makamanda wamemwambia kuwa linaweza kutokea Jumampili. Marekani inaendelea na shuguli ya uokoaji, lakini vikosi vya mwisho vya Uingereza , wanadiplomasia na maafisa kwa sasa wameondoka Kabul. Siku ya Alhamisi mlipuko wa bomu la kujitolea muhanga karibu na uwanja wa ndege uslisababisha vifo vya watu 170. Tawi la kieneo la Islamic State - katika jimbo la Khorasan (IS-K) -lilidai kuhusika na shambulio hilo.