Taarifa ya Habari 28 Septemba 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Hali ya wasiwasi yaongezeka jimboni Queensland baada ya dereva wa lori, aliye tembelea nakulala katika hoteli kadhaa kupatwa na COVID-19.


Serikali ya Victoria inalaumu maboresho ya programu kwa makosa ya utoaji wa matokeo ya vipimo, wakati jimbo hilo limerekodi kesi mpya 867 za maambukizi ya COVID-19, baadhi ya kesi zikiwa zime potea pamoja na vifo vinne. Takwimu hiyo ndiyo idadi kubwa ya kesi za kila siku tangu mwanzo wa janga na, kesi 140 za ziada ziliongezwa katika jumla ya kesi za Jumatatu, pamoja na maambukizi mengine tisa kwa takwimu za Jumapili.

Mashaka yame ibuka jimboni NSW kuhusu uwezo wama hospitali. Jimbo hilo lilirekodi maambukizi mapya 863 pamoja na vifo saba hii leo jumanne 28 Sep. Miongoni mwa vifo saba vilivyo ripotiwa, kulikuwa mwanamke mwenye miaka ya 90 aliyepatwa na COVID ndani ya hosptiali ya Nepean, na mwanamke mwenye miaka ya 70 aliyepata maambukizi hayo ndani ya hospitali ya Campbelltown. Brad Hazzard ni waziri wa afya jimboni NSW, amesema kuna ongezeko ya hatari yakulazwa hospitalini, punde amri yakubaki ndani itakapo inuliwa ila, hatua zinazo jumuishwa utoaji wa chanjo kwa wafanyakazi unatolewa kipaumbele.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezitaka serikali za mitaa kote nchini kushughulikia suala la Covid-19 kwa kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kupata chanjo na si kutumia mabavu. Ameyasema hayo leo Jumatatu katika mkutano mkuu maalum wa uchaguzi viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ngazi ya Taifa uliofanyika mkoani Dodoma. Kauli ya Rais Samia inakuja siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera kutaka watumishi wote wa afya mkoani huko, kuchanja huku akidai kuwa ni ngumu kwa watumishi wa afya ambao hawachanja kuwashauri wananchi kuchanja.


Share