Taarifa ya Habari 28 Novemba 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Kesi mbili za aina mpya ya kirusi cha UVIKO-19 kwa jina la Omicron, zime thibitishwa miongoni mwa wasafiri walio wasili jimboni New South Wales, kutoka Afrika Kusini Jumamosi 27 Novemba 2021.


Wawili hao walikuwa wame pata chanjo kamili na kwa sasa wako katika karantini ndani ya makaazi maalum ya idara ya afya. Idara ya Afya ya NSW, imesema wawili hao hawana dalili za uambukizi. Jana Jumamosi 27 Nov, serikali ya shirikisho ilitangaza kuwa wasafiri ambao si waakaji wa Australia kutoka nchi tisa za ukanda wa Kusini Afrika, watapigwa marufuku kuingia Australia, na wale ambao wame wasili hivi kariburni lazima waingie katika karantini kwa siku 14.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, amesema Ijuma kwamba “watawazika maadui”, akitoa ujumbe wake wa kwanza tangu kuwasili kwenye mstari wa mbele wa vita, kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa kundi la ukombozi wa tigray TPLF. Video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa twitter wa Abiy hii leo, inamonesha kiongozi huyo akiwa pamoja na viongozi wa jeshi katika eneo la mstari wa mebele wa vita. Katika mahojiano na televisheni ya Fana, Abiy ameonekana akiwa amevalia sare za kijeshi, Akizungumza katika lugha za Afaan Oromo na Amharic.

Tume ya kupambana na ufisadi ya Sierra Leone imewapata na makosa ya ulaji rushwa maafisa sita akiwemo mwanasiasa wa upinzani maarufu anayetarajiwa kugombea urais kwa tiketi ya vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2023. Samura Kamara alikuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha upinzani cha All People's Congress (APC) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2018. Vyama vya upinzani vimepanga kumteua kugombea urais katika uchaguzi ujao.


Share