Ikulu ya White House imekanusha madai kuwa rais Donald Trump aliarifiwa kuhusu ripoti ya kijasusi ilionesha kuwa Urusi ilitoa zawadi kwa wanamgambo wanaohusishwa na kundi la Taliban kwa mauaji ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amepinga kitendo cha kukamatwa kwa waziri wa sheria, akisema serikali ya mseto inaweza kuvunjika juu ya suala hilo na kumtaka rais kuwahakikishia mawaziri utetezi wa kisheria.
Kiongozi wa upinzani aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi wa marudio nchini Malawi Lazarus Chikwera ameapishwa kuingia madarakani.