Taarifa ya Habari 27 Juni 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Mkutano wa dharura wa kamati ya usalama wa Australia, utafanywa kesho Jumatatu 28 Juni 2021, kujadili milipuko ya COVID-19 nchini.


Serikali ya jimbo la Kusini Australia imesema inachukua uamuzi thabiti kuzuia usambaaji wa COVID-19, kwakufunga mipaka yake na Queensland, Magharibi Australia, Wilaya ya kaskazini na Australian Capital Territory maramoja.

Ni wakaaji tu wa kusini Australia na wasafiri muhimu, ndiwo watakao ruhusiwa kuingia katika jimbo la Kusini Australia kutoka maeneo hayo. Wakaaji wa New South Wales wanaendelea kupigwa marufuku kuingia jimboni humo, na wakaaji wa Victoria kwa sasa watahitaji kufanyiwa vipimo vya virusi hivyo siku yakwanza wanapo wasili jimboni humo.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema Ijumaa wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona limeikumba taifa na kwamba wagonjwa wa COVID-19 wapo. Rais ametumia nafasi hiyo pia kuwaomba viongozi wa dini nchini kutoa elimu ya kujikinga kwa waumini wao, ikiwemo kusisitiza wachukue tahadhari na kufuata ushauri unaotolewa na wataalam wa afya.


Share