Nchi 50 zimeidhinisha mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupiga marufuku silaha za nyuklia. Makubaliano hayo yatawezesha kuanza kutekelezwa kwa mkataba huo katika muda wa siku 90.
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amemkosoa vikali Rais Donald Trump na serikali yake hapo jana juu ya namna alivyoshughulikia janga la ugonjwa wa COVID-19 nchini humo, wakati wa hotuba yake mbele ya wafuasi wa mgombea urais wa Democratic Joe Biden.
Kutangazwa kwa mapendekezo ya marekebisho ya katiba nchini Kenya kupitia ripoti ya jopo la maridhiano maarufu kama BBI ili kupanua serikali, kunaendelea kupokea hisia mbalimbali na maoni mseto kutoka kwa raia wa Kenya, makundi na mashirika mbalimbali.