Taarifa ya Habari 25 Julai 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Viongozi wa New South Wales na Victoria, wakosoa vikali raia walio shiriki katika maandamano dhidi ya makatazo na vizuizi vya COVID-19 mjini Melbourne na Sydney.


Jimbo la New South Wales limerekodi kesi mpya 141 za COVID-19, na kesi 38 kati yazo zikiwa ni watu ambao wako katika hali ambukizi ndani ya jamii.

Waziri Mkuu wa Australia, Scott Morrison amesema ni 16% tu yawatu wanao stahiki kupata chanjo za COVID-19, ndiwo wame pata chanja kamili. Ila, ni 37% ya moja ya kundi lawa Australia ambao wako hatarini zaidi, hususan wenye zaidi ya miaka 70, ambao wame pata dozi zote mbili.

Watu kumi na sita wameuawa na wengine zaidi ya nane kujeruhiwa na waasi wanao dhaniwa kuwa wapiganaji wa kikundi chenye msimamo mkali wa kidini cha ADF ambao walishambulia lori moja la abiria. Shambulizi hilo limetokea katika njia kuu kati ya miji ya Maimoya na Chani-chani, kiasi cha kilomita 40 kutoka mji wa Beni, jimbo la Kivu Kaskazini.


Share