Taarifa ya habari 25 Aprili 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Ibada zimefanyika hii leo kuadhimisha mwaka wa 106, wa vikosi vya Australia na New Zealand kutua katika eneo la Gallipoli nchini Uturuki.


Sherehe za umma zilifanyika kwa mara ya kwanza tangu 2019, kwa sababu ya janga la COVID-19.

Waziri Mkuu Scott Morrison na balozi wa New Zealand Dame Annette King, waliweka shada za maua katika sehemu ya kumbukumbu ya vita yakitaifa ya Canberra, kuadhimisha Anzac Day. Na katika upande wa pili wa Tasman, waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern, alitoa heshima zake kwa maisha yawalio hudumu kwa niaba ya Australia na New Zealand. Bi Ardern alitoa heshima zake kwa wanawake katika jeshi la ulinzi la nchi yake.

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amelihutubia bunge la Tanzania kwa mara ya kwanza Alhamisi tangu achukue urais mwezi uliopita baada ya kifo cha mtangulizi wake John Magufuli. Rais akizungumza katika Bunge mjini Dodoma, ametumia muda mrefu kuzungumzia mbinu mbali mbali za ukuzaji uchumi na pia kutangaza kuwa atakutana na viongozi wa vyama vya siasa nchini humo kujadili mwelekeo mpya wa demokrasia baada ya miaka sita ya vyama vya upinzani kulalamika kuwa vinabanwa kidemokrasia.


Share